Jifunze jinsi ya kutumia IFS() katika Excel ili kufanya maamuzi kulingana na masharti mengi kwa urahisi. IFS() inarahisisha kazi ya nested IF na kufanya data yako kuchambuliwa kiotomatiki.

FORMULA NA MAELEZO YA KIUNDA:

=IFS(A1>90, "A", A1>75, "B", A1>60, "C", A1>50, "D", A1<=50, "F")


IFS() ni formula ya Excel inayotumia masharti mengi bila kuhitaji nested IFs.

A1>90, "A" – ikiwa sharti la kwanza limekamilika, matokeo ni “A”

A1>75, "B" – ikiwa sharti la kwanza halikamiliki, lakini hili limekamilika, matokeo ni “B”

Unaweza kuongeza masharti mengine kwa kuendelea kuongeza pairi za sharti + matokeo

Rahisi kukumbuka: “IFS = Ikiwa sharti1, toa matokeo1; ikiwa sharti2, toa matokeo2;…”

Faida: Inarahisisha masharti changamano, inafanya spreadsheet kuwa safi na rahisi kusoma.

LINKS NA RESSOURCES:

Tazama tutorials zaidi za Excel: https://www.faulink.com

Download mifumo ya Excel bure: https://www.faulink.com/excel_mifumo.php

Msaada wa WhatsApp: https://wa.me/255693118509