FAUSTINE May 12, 2025 1 min read

Database ni Nini? Tambua Umuhimu Wake na Mifano Katika Teknolojia ya Kisasa

Database ni mkusanyiko wa taarifa zilizopangwa vizuri na kuhifadhiwa kwa njia ya kielektroniki ili ziweze kupatikana, kusomwa, kuongezwa au kufutwa kwa urahisi. Database hutumika katika programu nyingi kama mifumo ya shule, hospitali, benki, maduka na hata mitandao ya kijamii.

Mfumo wa database husaidia katika kutunza taarifa kama majina ya wanafunzi, malipo ya wateja, hesabu za bidhaa, na rekodi nyingine muhimu. Lugha maarufu ya kuwasiliana na database ni SQL (Structured Query Language).

Mifano ya Database Maarufu:

MySQL – hutumika sana kwenye PHP na WordPress.

Oracle – hutumiwa na mashirika makubwa.

MongoDB – database isiyo na muundo wa jedwali (NoSQL).

Microsoft SQL Server – hutumiwa katika mifumo ya kampuni kubwa.

Firebase – hutumiwa katika apps za simu.

🚀 Unahitaji mfumo au website ya biashara?

Chagua huduma hapa chini kisha mteja bofya moja kwa moja kwenda kwenye ukurasa wa huduma au kuwasiliana nasi kwa WhatsApp.

Share this post

Comments

0
No comments yet. Be the first to comment.

Continue Reading

Subscribe

Get new updates

Jiunge upokee posts mpya, tutorials, na updates za mifumo moja kwa moja kwenye email yako.

Faulink Support