Cybercriminals siku hizi wanatumia njia nyingi kuwadanganya watu ili wawape taarifa muhimu. Mara nyingi hutuma barua pepe (emails), SMS, links, au social media messages wakijifanya ni taasisi halisi kama benki, kampuni ya simu au tovuti unazoamini.

Hapa chini ni mbinu rahisi lakini muhimu za kutambua phishing emails na scams mtandaoni.

✅ 1. Angalia Sender Email Address (Mtumaji Halisi au Feki?)

Wahalifu hutumia barua pepe zinazofanana na za kampuni halisi:

support@crdb-support.com badala ya support@crdbbank.co.tz

info@facebook-security.net badala ya security@facebook.com

🔍 Tip: Angalia domain ya email kwa makini, mara nyingi kuna spelling errors.

✅ 2. Viungo (Links) Vinavyotumwa – Hover Kabla ya Kubofya

Usibofye link kama hujaithibitisha.
Bonyeza juu ya link bila kubofya (hover) kisha uangalie:

Inapeleka kwenye domain halisi au feki?

Mfano:

HALISI: https://bank.crdbbank.co.tz/login

FEKI: https://crdbbank-secure-login123.xyz

🔐 Tip: Kamwe usiingize password kwenye link isiyo rasmi.

✅ 3. Ujumbe wa Haraka (Urgency / Panic Messages)

Scammers hutumia vitisho kama:

“Akaunti yako itafungwa ndani ya saa 24!”

“Bofya hapa uepuke kufutwa!”

“Umeshinda zawadi, thibitisha mara moja!”

🎭 Wahuni wanataka uchanganyikiwe ili ukubali kuingia kwenye mtego.

✅ 4. Spelling & Grammar Errors

Kampuni kubwa huwa hazitumi barua pepe zenye makosa mengi ya:

Sarufi

Maneno yasiyoeleweka

Sentensi zisizo na mpangilio

📌 Makosa mengi = ishara ya phishing.

✅ 5. Mafaili ya Ajabu (Attachments)

Attachments kama:

.exe

.zip

.html

.scr

…mara nyingi huambukiza kompyuta yako malware, ransomware au spyware.

📛 Usifungue attachment kama haikuombwa na haijulikani.

✅ 6. Omba Password, PIN, au ATM Taarifa

Taasisi halisi HAIWAI kuomba:

PIN ya ATM

Password ya email / system

CVV ya kadi

OTP (one-time password)

🥷 Uki dimandishwa kutoa taarifa hizi → 100% SCAM.

⚠️ 7. Phishing Kupitia Social Media

Wahalifu hutumia:

Facebook Messenger

WhatsApp

Instagram

TikTok

Scams maarufu:

Link za “angalia video yako”

Link za “umeonekana kwenye video hii”

Logs za giveaways feki

🛡️ Jinsi ya Kujilinda Dhidi ya Phishing
✔️ Tumia 2FA (Two-Factor Authentication)

Hata ukiibiwa password, akaunti yako bado itakuwa salama.

✔️ Tumia Password Manager

Inazuia kuingia password kwenye tovuti za feki.

✔️ Update apps & browsers mara kwa mara

Updates hulinda dhidi ya malware mpya.

✔️ Epuka kutumia public WiFi kwa login za benki
✔️ Tumia antivirus & firewall
🔐 Dalili za Haraka za Phishing Email

Email inakuomba ubonyeze link haraka

Inakuomba confidential info

Kutoka kwa mtu au kampuni isiyojulikana

Spelling errors nyingi

Muundo wa ajabu (logo feki)

Link inayoelekeza kwa domain ndefu isiyo ya kawaida

💬 Ukishukiwa Email Ni Phishing, Fanya Hivi

Usibofye link yoyote

Usifungue attachment

Ripoti kwa IT au security team

Futa email mara moja

Badilisha password kama uliwahi kubofya link

🔗 Links Za Kujifunza Zaidi

🌐 Faulink Official Website
https://www.faulink.com

📘 Jifunze Cybersecurity, Coding & Web Design
https://www.faulink.com/excel_mifumo.php

📲 WhatsApp Support
https://wa.me/255693118509