Jifunze Excel XLOOKUP(): Kutafuta Data Haraka na Rahisi
1. XLOOKUP() Function
XLOOKUP() ni function ya lookup inayoweza kutafuta thamani kila upande, yaani kutoka column au row, na kurudisha matokeo kwa urahisi. Ni mbadala bora zaidi ya VLOOKUP na HLOOKUP.
Syntax:
XLOOKUP(lookup_value, lookup_array, return_array, [if_not_found], [match_mode], [search_mode])
lookup_value = thamani unayotafuta
lookup_array = range ya data unayotafuta ndani yake
return_array = range ya data unayotaka kurudisha matokeo
if_not_found = thamani ya default ikiwa lookup_value haipo
match_mode = 0 (exact match, default), -1 (exact or next smaller), 1 (exact or next larger), 2 (wildcard match)
search_mode = 1 (first to last, default), -1 (last to first)
2. Mfano Rahisi
Mfano 1: Tafuta jina la mteja kulingana na ID
ID Name
101 John
102 Mary
103 Ali
Formula:
=XLOOKUP(102, A2:A4, B2:B4, "Not Found")
Result: Mary
XLOOKUP inatafuta 102 kwenye column A2:A4 na kurudisha value kutoka B2:B4.
3. XLOOKUP() Badala ya VLOOKUP
Hakuna column index number, unachagua direct return_array.
Inafanya lookup kutoka column yoyote bila kuhitaji kuwa column ya kwanza.
Ina option ya if_not_found badala ya kutumia IFERROR().
Mfano:
=XLOOKUP(105, A2:A4, B2:B4, "Not Found")
Result: Not Found
4. Kutumia XLOOKUP() Pamoja na AND()/OR()
Mfano: Angalia stock ya bidhaa na status
=IF(OR(XLOOKUP(C2, ProductList!A2:A10, ProductList!C2:C10,0)=0, XLOOKUP(C2, ProductList!A2:A10, ProductList!B2:B10,0)="Out of Stock"), "Not Ready", "Ready")
C2 = Product ID
ProductList!A2:A10 = Product IDs, B2:B10 = Status, C2:C10 = Quantity
5. Tips Muhimu
XLOOKUP() ni rahisi, flexible, na inasuluhisha matatizo yote ya VLOOKUP/HLOOKUP.
Inaweza kuunganishwa na IFERROR(), IF(), AND(), OR(), SWITCH(), INDEX(), MATCH() kwa reports changamano.
Inaruhusu lookup kwa rows au columns, na ina default result ikiwa thamani haipo.
Links Muhimu
Tazama tutorials zaidi za Excel: https://www.faulink.com
Download mifumo ya Excel bure: https://www.faulink.com/excel_mifumo.php
Msaada wa WhatsApp: https://wa.me/255693118509