Jifunze jinsi ya kuhesabu seli ambazo hazina data yoyote katika Excel. Hii ni muhimu unapohitaji kuona ni seli ngapi bado hazijajazwa kwenye ripoti yako.

FORMULA NA MAELEZO YA KIUNDA:

=COUNTBLANK(A1:A10)


COUNTBLANK ni formula ya Excel inayohesabu seli zote tupu katika safu uliyochagua.

A1:A10 inawakilisha safu au seli unazotaka kuhesabu; badilisha kwa safu yako.

Formula hii haitahesabu seli zilizo na nambari, maandiko, au tarehe; inahesabu tu seli zilizo wazi kabisa.

Rahisi kukumbuka: “COUNTBLANK = Hesabu Seli Tupu”.

Unaweza pia kutumia kwa safu kubwa zaidi, mfano: =COUNTBLANK(B2:F20) ili kuona seli zote ambazo bado hazijajazwa.

LINKS NA RESSOURCES:

Tazama tutorials zaidi za Excel: https://www.faulink.com

Download mifumo ya Excel bure: https://www.faulink.com/excel_mifumo.php

Msaada wa WhatsApp: https://wa.me/255693118509