Jinsi ya Kutengeneza Payment Link ClickPesa Step by Step
Jinsi ya Kutengeneza Payment Link ClickPesa Step by Step
Ingia kwenye dashboard ya ClickPesa.
Kwenye menu ya kushoto, bonyeza Payment Pages.
Bonyeza Create au Create Payment Page.
Kwenye Page Name, andika jina la malipo.
Mfano: Ada ya Shule, Malipo ya Bidhaa, au Michango.
Kwenye Amount, chagua currency TZS, kisha andika kiasi.
Mfano: 10000.
Kwenye Page Image, unaweza kuweka picha ya bidhaa, logo, au tangazo. Hii si lazima.
Bonyeza + Add description kama unataka kuongeza maelezo.
Mfano: Lipa ada ya shule kwa njia ya simu.
Bonyeza Create Page.
Baada ya page kutengenezwa, ClickPesa itakupa payment link.
Copy link hiyo kisha tuma kwa mteja kupitia:
WhatsApp
SMS
Email
Facebook
Website yako
Mteja akifungua link, ataona ukurasa wa malipo na kuchagua njia ya kulipa kama M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa au njia nyingine zinazopatikana.
Mfano wa kujaza:
Page Name: Malipo ya Ada
Amount: 20000 TZS
Description: Tafadhali lipa ada yako kwa kutumia namba yako ya simu.
Baada ya malipo kufanyika, utaona taarifa kwenye Transactions.
🚀 Unahitaji mfumo au website ya biashara?
Chagua huduma hapa chini kisha mteja bofya moja kwa moja kwenda kwenye ukurasa wa huduma au kuwasiliana nasi kwa WhatsApp.